Hiki Ndiyo Kitu Pekee Kitakachokupa Furaha Ya Pekee Ukifanikiwa Kukifanya.


Categories :


Mafanikio maishani yanapatikana kwa kufanya vitu na sio kuweka mipango au kusema peke yake.

Licha ya kuweka kazi katika maisha yako lakini umeendelea kupata mafanikio ya kawaida ambaye yanakupelekea kuwa na maisha ya kawaida. Ndiyo maana matokeo ambayo umekuwa ukiyapata yamekuwa hayakushangazi wewe wala mtu mwingine.

Licha ya mafanikio uliyoendelea kuyapata lakini bado hujapata ridhiko kama kweli umepata kitu kikubwa maishani mwako. Licha ya kupiga hatua lakini hujaridhika na kuona kuna kitu cha maana ambacho umekifanya. Hata ukifikiria kufa leo unaona bado dunia inakudai. Hii yote ni kwa sababu hujafanikiwa kufanya kitu muhimu sana katika maisha yako. Kitu hicho ni kile ambacho wengine wamesema hukiwezi.


Kwa sababu ya watu waliokuzunguka, umekuwa ukifanya vitu ambavyo kila mtu atakuambia unaweza kukifanya. Ndiyo maana hakuna hata mmoja ambaye amekuwa akishituka au kukukatalia pale ambapo umekuwa ukishirikisha mipango yako maisha yako. Hii yote ni kwa sababu umekuwa ukifanya vitu vya kawaida. Ndiyo maana hata mafanikio yalipokuja hayajashitua moyo wako na kukipa furaha ya utofauti.

Furaha na ridhiko lipo kwenye kupata matokeo yale ambayo watu waliokuzunguka walikataa na kuona huwezi kuyapata, na mara nyingine hata wewe mwenyewe uliona kama ni kitu kisichowezekana. Kuweka malengo ya kawaida yatakupa matokeo ya kawaida. Lakini ili upate matokeo makubwa zaidi na ya kushangaza huna budi kuwa na kitu kikubwa kwanza unachokifanyia kazi.

Moja ya kitu kikubwa unachoweza kukifanyia kazi ni kikakupatia majibu ya makubwa, yakushangaza na ya furaha kubwa ni kuishi ndoto kubwa ya maisha yako. Ndoto kubwa hushtua mtu mwingine anapoelezwa. Ndoto kubwa hubeba matokeo makubwa. Ndoto kubwa huchukua muda mrefu wa maisha yako.

Ndoto kubwa hutengenezwa kutoka kwenye vitu unavyovipenda kufanya. Huko ndiko unakoweza kutengeneza lengo kubwa la maisha yako ambalo unatamani litimie kabla hujaondoka hapa duniani. Kwa sababu ndoto yako itatoka kwenye kile unachopenda kukifanya, hii inamaanisha kuwa utaanza kupata furaha kubwa tangu kwenye mchakato wake. Hii ni kwa sababu ya imani ambayo utakuwa nayo ambayo itakufanya uwe unayaona matokeo hata kabla hujayapata.

Kitu gani kinaweza kutawala akili yako usiku na mchana? Kitu gani unakiona unaweza kukitimiza hata kama watu wanaokuzunguka ikiwepo watu wa karibu yako wakuambua huwezi? Je kufikia kiasi fulani cha fedha ambacho kitakupa uhuru wa kifedha? Je ni kuiondoa hali fulani kwenye jamii inayowatesa watu kwa muda mrefu?

Muda umefika sasa wa kuanza kuishi ndoto kubwa na kuacha kuishi ndoto ndogo za kawaida ambazo matokeo yake hayakupi ridhiko la moyo wako. Kitu kimoja ambacho inabidi ukifahamu na kitakachokupa nguvu ya kuishi ndoto kubwa badala ya ndoto ndogo ni kuwa muda wa kuishi ndoto ndogo ni sawa na ule wa kuishi ndoto kubwa na mara nyingine hata nguvu. Chagua kuishi ndoto kubwa sasa.


Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *