Unataka Matunda Mapya? Badili Kwanza Mizizi.


Categories :



Kuna hatua fulani ya maisha imekuchosha na hutamani kuendelea katika hali hiyo. Je ni umasikini? Au afya mbovu? Kuna tabia fulani ambayo umekaa nayo kwa muda mrefu sasa na unaichukia. Mara nyingi umetamani ubadili hali hizo, lakini licha ya majaribio hayo, hali hiyo ipo pale pale.

Kile ambacho umekuwa ukikifanya bila kupata matokeo ni kujaribu kupata matunda tofauti bila kubadili mizizi yake. Itakuwa ajabu kuurudia kesho mti uliochuma matunda ya limau leo ukitarajia kupata machungwa. Huwezi kupata matunda tofauti kama hutabadili kinachozalisha matunda hayo. Kukaa na kuja kuchuma matunda ya muda ule ule, haibadili matunda yanayopatikana kwenye mti huo.


Licha ya watu kukasirishwa na hali fulani, lakini tumekuwa watu wamekuwa wakiendelea kutarajia kuwa labda hali hizo zitabadilika bila kuchukua hatua sahihi. Kulalamika hakubadili kipato chako na kukutoa kwenye umasikini, kusikitika tu kwa uzito wa ziada ulionao pekeyake hauwezi kukuepusha na hatari ya magonjwa. Kutamani kuwahi kuamaka pekeyake hakuwezi kukakuinua kitandani mapema asubuhi. Ukitaka matunda mapya, badili kwanza mizizi.

T. Harv Eker alisema “If you want to change the fruits, you will first have to change the roots. If you want to change the visible, you must first change the invisible” akimaanisha kuwa kama unataka kubadili matunda, unatakiwa ubadili mizizi kwanza. Ili ubadili vinavyoonekana, ni lazima ubadili visivyoonekana. Kabla hujahangaika na kubadili na vile vitu vinavyoonekana, kuna hatua moja nyuma ya kubadili kwanza visivyoonekana. Vitu visivyoonekana ni mawazo ambayo yanazaa mtazamo na tabia.

Mitazamo na tabia ndiyo vinavyozaa matunda ya maisha yako. Hii ni kwa sababu chochote kinachoonekana kwa macho kilianza kama wazo liliojenga mtazamo ambao unauishi kama tabia. Kumbe ili uweze kufanya mabadiliko ya kweli na kupata matokeo tofauti, huna budi kuanza na kubadili mtazamo wako na tabia zako kuhusu hali hiyo.

Kama tatizo linalokusumbua nia kipato kidogo, lazima uanze kwanza kubadili mtazamo wako kuhusiana na njia za kipato unazotumia sasa. Je una mawazo gani kuhusu mifereji mingine ya kipato? Je una mtazamo gani kuhusu thamani na kipato? Kama huna mawazo sahihi kuhusu maeneo hayo itakuwa ni vigumu kufanya maamuzi sahihi ya kuuliza kipato chako.

Kama hali inayokukumba sasa ni uzito wa mwili wako uliopitiliza ambao utasababisha magonjwa, huwezi kubadili chochote mpaka uwe na mtazamo sahihi. Je umejenga tabia ya kujinyima kula baadhi ya vyakula kwa sababu vinaongeza uzito sana na kuhatarisha afya yako.

Naamini kuna hali unazopitia sasa ambazo usingetamani kuendelea kuishi nazo. Lakini umeendelea kuishi nazo kwa sababu ya kutobadili mizizi yake ambayo ni mitazamo yake. Kwenye kila hali weka bayana mizizi yale na anza kubadili huko kwanza.

Kwenye utajiri: Amini kuwa utajiri ni mzuri. Amini kuwa kuana utele. Weka mizizi ya akiba. Ona thamani ndiyo utajiri.

Kwenye afya: Badili mizizi ya mlo, mazoezi na muda wa kupumzika.

Kwenye mahusiano: Boresha hali yako ya sasa kwa kubadili mizizi muda maalumu na washirika, upendo, kujali na thamani.

Kwenye maendeleo binafsi: Jenga mizizi sahihi ya mtazamo, mawazo yanayoingia akilini mwako na ndiyo yanayoamua uwe nani.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *