Hivi Ndivyo Unavyomaliza Mafuta Ya Gari La Safari Yako Hapo Duniani.
“Gari lililowasha na kuendelea kuunguruma bila ya kuondoka litaendelea kutumia mafuta hata baadaye mafuta kuisha kabisa”
Chochote unachoweza kukifanya hapa duniani kimeunganisha na muda. Kama huna muda huwezi kufanya chochote. Baada ya kufa muda na maisha yako hukoma pale kwani hutaweza kufanya kitu chochote. Licha mtu anaweza kufa muda wowote lakini umri wa uzeeni ndiyo huwatia watu wasiwasi mkubwa kwani hujua muda wao wa kufanya vitu umebaki kidogo sana. Hivyo historia ya maisha yako huandikwa kipindi cha uhai wako baada ya hapo huna muda wa kuandika historia yoyote.
Dunia imekuwa na usawa kwenye muda. Kila mtu ana masaa ishirini na nne kwenye siku
Hakuna aliyepunguziwa wala kuongezewa hata sekunde moja. Kumbe utofauti wa mafanikio ambao watu wanao ni kwa namna gani wanatumia muda huo sawa.
Vitu unavyovifanya kila siku ndivyo vinavyoamua upate nini katika maisha yako. Je siku yako huwa inaishaje? Limbuka kila siku inapoisha unakuwa umepunguza muda wako wakuishi hapa duniani. Je kama muda ndiyo mafuta ya kukufikisha kwenye mafanikio ya maisha yako ya hapa duniani, siku inapoisha unakuwa umetembea maili ngapi kuelekea mwisho wa safari yako?
Kumbuka una muda wa kufanya kila kitu kulingana na vipaumbele vyako. Ukiona hufanyi kitu fulani, si kwa sababu huna muda bali si kipaumbele chako. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuwa muda hautoshi kufanya mambo, mambo ni mengi sana, lakini licha ya kuwa busy hivyo bado kumekuwa na tatizo kwenye la kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio yale mtu anayostahili. Yaani kama ni gani ni kuwa linaendelea kuunguruma huku likila mafuta bila ya kuondoka hapo lilipo.
Bahati mbaya au nzuri ni kuwa, hata pale unakuwa hufanyi jambo fulani si kwamba muda utasimama ili ukusubiri uwe tayari. La hasha! Ndiyo maana mara nyingine umekuwa ukijiambia mwenyewe kuwa muda unakimbia kweli! Ni kweli unakimbia kwa sababu haujawahi kusimama hata kwa sekunde moja.
Unapoweka malengo na kutoyafanya kisha kufanya mambo mengine muda husimama. Unapopanga kufanya jambo kisha kuliahirisha, muda hautasimama. Unapoacha kazi kulalamika, kupiga udaku, kubishana au kubishana muda hautasimama umalize hayo na kuanza kutembea tena baada ya wewe kurejea kazini. Huku ni kuruhusu gari kuendlea kuunguruma na kula mafuta bila ya kuondoka. Muda hautasimama ukusubiri wewe uhangaike na fursa kisha urudi kwenye jambo la kwako uliloliacha kwa tamaa ya fursa mpya.
Chukua hatua: Tambua kitu ambacho umeamua kukomaa nacho kisha tembea na muda huku ukikifanya hicho bila kuacha. Acha fursa zipite, uliyoyashikilia kwa sasa yanatosha. Unachagua kukaa na nini?
Ndugu! Baada ya kumaliza mafuta ya maisha yako, Mtandao wa Amsha Uwezo unakushauri ujiunge na kundi maalumu la wasap (Amsha Uwezo). Hili ni kundi litakalokusaidia kutumia muda wa maisha yako vizuri kwa kukupa maarifa na miongozo sahihi ya kukusaidia kuchukua hatua sahihi kila siku na kupiga hatua kubwa katika maisha yako. Si hivyo tu bali mtandao huu utakupa ushauri na usimamizi kuhakikisha unatumia muda wako vizuri ili siku inapoiisha uwe umepiga hatua. Kama haitoshi Amsha uwezo itakuunganisha na watu wengine wenye hamu kubwa ya kupiga hatua na hivyo kuambukizana hamasa itakayokuwezesha kupendelea kuchukua hatua hata pale unapokutana na magumu.
Gharama za kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000) ambayo unaweza pia kulipia kwa awamu mbili. Hii sio fursa ya kujiuliza mara mbili, jiunge sasa na kuanza kufaidi makubwa yaliyopo. Kujiunga na mtandao bonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD
Kwa mawasiliano zaidi usisite kuwasiliana nami kupitia simu 0752206899/0714301952.
Asante.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz