Utapata Unachokitaka Kuanzia Sasa.
Ni muda umepita tangu umezaliwa, ni muda mrefu tangu umehitimu masomo yako, ni muda mrefu tangu umeondokewa na wategemezi wako, ni muda mrefu umepita tangu umeanzisha biashara lakini hujaanza kupata faida; hali hizi zimekufanya ujisikie kama umefika mwisho kwani huoni nini ufanye ili usonge mbele.
Sasa nifanye nini? Ninaanzia wapi? Haya ni maswali unayojiuliza baada ya kutoanza jambo fulani kwa muda mrefu au kukwama kupiga hatua zinazoonekana baada ya kuweka nguvu kwenye jambo hilo kwa muda mrefu. Utaanzia wapi ili kutoka kwenye hali kama hiyo?
Si kweli kwamba ukiwa katika hali ya kukwama unakuwa huna sehemu ya kuanzia, la hasha! Nini cha kufanya huwepo lakini wengi hushindwa kuona nini cha kufanya baada ya akili zao kubaki zimeshikiliwa na kumbukumbu za yale yaliyokufikisha hapo ulipo. Hizi ni kumbukumbu zinazokupa maumivu kadri unavyokumbuka. Hizi ndiyo kumbukumbu zilizojaza mawazo hasi na hivyo kukosa nafasi ya mawazo chanya. Lakini katika mazingira kama hayo, maisha yako mafanikio yanaanzia hapo ulipo yaani hapo ulipofikia.
Ulipo sasa kunatengeneza mwanzo mwingine wa maisha yako yajayo. Bila kujali kile ambacho hujakianza wala kukitengeneza kwa muda mrefu. Bila kujali ugumu ambao umekutana nao katika safari ya awali, sasa unaweza kutengeneza mwanzo mwingine mpya wa maisha yako.
Kabla hujafa unaweza kuanza maisha mapya na kufikia mafanikio makubwa. Kama unasoma hapa inaonyesha kuwa wewe bado u hai na hivyo unaweza kuanza maisha mengine na kufikia mafanikio yako makubwa hata kama unaona umechelewa.
Bado una nafasi. Kuna methali ya Kichina inasema muda wa kupanda mti wa kivuli ilikuwa miaka ishirini iliyopita lakini kama hukufanya hivyo, muda mwingine mzuri ni leo. Kuna maisha uliyotarajia uyajenge mpaka sasa, lakini hayajatimia, inawezekana ilibidi ufanye hivyo miaka kadhaa iliyopita, lakini kama ulishindwa fanya hivyo sasa.
Rekebisha makosa. Njia pekee ya kufaidika na makosa yako ni kujifunza kutokana na makosa hayo. Upo hapo ulipo kwa sababu ya makosa kadhaa uliyoyatenda. Lakini ukitambua kosa hilo na kuweka usahihi wake hutapata matokeo ya awali. Ulikosea wapi, usikate tamaa badala rekebisha na kuanza au kuendelea kwa usahihi.
Usiumizwe na historia. Makosa uliyoyafanya yasikuumize sasa. Usiendelee kuyakumbuka hayo kiasi cha kushindwa kuyaishi maisha yako ya sasa. Huwezi kubadili chochote kwenye yale yaliyopita. Akili na moyo wako ikumbatie mambo ya sasa vikitazamia vijavyo.
Komboa wakati. Kuna wakati umeshaupoteza, huna muda mwingine wa kuendelea kupoteza. Hakikisha unautumia muda wowote wa uhai wako utakaoupata. Pangilia vizuri kazi unazotaka kuzifanya kisha weka nidhamu kubwa kuhakikisha unazitimiza.
Usiwaangalie wengine. Inawezekana kuna watu umezaliwa nao, ukiwaangalia mafanikio makubwa waliyoyapata inakukatisha. Katika nyakati hizi huna budi kujilinganisha na mtu mwingine bali kile ulichostahili kukifanya lakini hujafanikiwa. Baada ya hapo weka nguvu kutimiza hivyo.
Ndugu yangu! Huu sio wakati wa kunyoosha mikono kuashiria umeshindwa, bali kuzaliwa upya ili kuweka nguvu zaidi ili kutimiza yale uliyoyatamani muda mrefu.
Mtandao wa Amsha Uwezo unaamini una uwezo mkubwa ndani yako uliolala tu ambapo ukiamshwa utaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya uliyoyapata sasa. Nakushauri ujiunge na kundi maalumu la wasap la Amsha Uwezo ili uamke tena. Kupitia mtandao huu utapata
1. Miongozo mbalimbali ya kukuwezesha kufanya vitu kwa usahihi zaidi kama vile kuweka na kutimiza malengo.
2. Makala na maarifa mbalimbali ya kukuwezesha kukabiliana na changamoto
3. Ushauri mbalimbali kutoka kwangu mwalimu wako pale unapokuwa unakwama
4. Usimamizi mbalimbali utakaokulazimisha kuchukua hatua
5. Kuwa na watu sahihi kwenye kundi wenye nia ya kupata mafanikio kama wewe hivyo kupata hamasa ya kudumu.
Gharama za kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000) . Hii ni ofa kwako ukilinganisha na thamani kubwa unayoenda kuipata. Jiunge leo kupitia kiunganishi hapo chini ili uanze kufaidi mambo makubwa. Kwa maelezo zaidi piga simu 0752 206 899. Karibu. Bonyeza hapa kujiunga;
https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz