Umeshindwa Si Kwa Sababu Ya Kutokufahamu, Ila Kwa Sababu Hii…


Categories :



Ni muda mrefu sasa tangu umekuwa na matamanio ya kupata mafanikio fulani katika maisha yako. Ni muda sasa tangu ulipohamasika kuchukua hatua fulani lakini baada ya hapo shauku hiyo imekuwa ikishuka kila siku, na mpaka sasa hakuna ulichokifanya. Ni muda mrefu umepita tangu umekuwa na wazo la kuanzisha au kukuza biashara lakini kila siku unasema kesho.

Ni jambo linalokuumiza sana. Imefika hatua unafikiri kuwa umelogwa au una nuksi. Kwa sababu ya kutokuwa na matokeo wakati unafahamu hatua za kuchukua ni sawa na kutokufika safari wakati njia ya kuifikia safari hiyo unaifahamu.



Lakini kwenye kila jambo linalotokea kuna visababishi. Hivyo kwa matokeo unayoyapata, kuna visababishi vinavyotokea. Hivyo usishangae imekuwaje bali jiulize nini kinasababisha haya yote? Kwa nini huna matokeo ingali unajiona una uwezo? Lakini kuna sababu nyingi ambazo si kwa sababu ya ufahamu bali kutofanya vile ambavyo tayari unavifahamu;

Unayoyafahamu lakini hujayafanyia kazi: Kuna maarifa mengi ambayo unayoyafahamu lakini hujaanza kuyatumia. Kwa mfano;
A. Unafahamu kuwa ili uweze kupata mtaji na kuwekeza inabidi uweke akiba kwenye kila kipato, angalau 10%. Je unafanya hivyo?
B. Unatambua kabisa ili uweze kuianza siku yako vyema huna budi kuamka mapema na kuipangilia siku yako,
kufanya mazoezi, kutafakari kuhusu maisha yako. Je unaamka saa ngapi?

Kama unaahirisha unajua unachotaka kufanya. Kuahirisha ni kitendo cha kutokufanya sasa au muda fulani uliopangwa mpaka muda mwingine. Kwa mantiki hiyo mtu huahirisha vitu anavyovifahamu na alivyotakiwa kufanya. Hii imekuwa ni sababu kubwa ya kutopata matokeo. Katika hili huna kitu kingine cha kufahamu zaidi ya kuanza kufanya kwa wakati.

Kama unasema maisha magumu unafahamu nini ukifanye. Utajua kama maisha ni magumu baada ya kuchukua hatua na kukutana na ukinzani. Unapokutana na ukinzani unahitaji kupata maarifa zaidi, kuweka nguvu zaidi, kupata hamasa zaidi. Badala ya kulalamika maisha magumu, fanya kile kinachotakiwa.

Ndugu! Kuna hatua ya kufanya baada ya kufahamu nini unachotakiwa kufanya. Umekwama hapo si ulipo kwa muda mrefu, si kwa sababu hujui nini ukifanye bali hufanyi kile unachokifahamu. Kwa kutambua hilo, mwalimu wako nakushauri ujiunge na kundi maalumu la wasap (Amsha Uwezo). Kwa wewe kuwa kwenye kundi hili utapata fursa ya kwenda zaidi ya kujua kwa kukuwezesha kuchukua nafasi. Hii inawezekana kusimamiwa na kupata hamasa ya kudumu. Kupitia kundi utafanikiwa kuanza kuchukua hatua uliziahirisha siku nyingi na kutumia maarifa unayoyafahamu.

Anza sasa kufanyia kazi unayoyafahamu ili kupata matokeo.

Gharama za kujiunga na kundi hili ni shilingi elfu kumi (Tsh 10,000) . Hii ni ofa kwako ukilinganisha na thamani kubwa unayoenda kuipata. Jiunge leo kupitia kiunganishi hapo chini ili uanze kufaidi mambo makubwa. Kwa maelezo zaidi piga simu 0752 206 899. Karibu. Bonyeza hapa kujiunga;
https://chat.whatsapp.com/Dx1HF02stFq2LxIqoRTAUD


Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *