Pandisha Ngazi Kupanda Kileleni.


Categories :



Hatua ya mafanikio ya maisha uliyofikia ni kwa sababu ya viwango ulivyojiwekea maishani mwako. Viwango hivyo ndiyo ndivyo vinavyoamua ufanikiwe kiasi gani kwenye kila nyanja ya maisha yako.  Viwango hivyo ndivyo vinavyoweka ukomo kwenye  mafanikio unayoyapata, hii ndiyo sababu ya kwa nini muda umezidi kwenda lakini bado upo pale pale.

Viwango hivyo ulivyojiwekea vimeanzia kwenye akili yako. Kile ambacho unakiamini kuwa unastahili na unaweza kukipata ndicho unachokipata maishani. Kama akili yako inaamini wewe ni viwango vya laki, inakuwa ngumu sana kupata milioni. Hata ikatokea kwa bahati mbaya ukapata milioni, suala la muda, utarudi tena kwenye kiwango cha laki. Kama akili yako haiamini kuwa unaweza kuwa bilionea, basi jitihada zote zitakuwa zinaishia kwenye milioni.
Ndiyo maana kuna watu wamewahi kupata fedha nyingi kwa mkupuo ambazo zilikuwa juu ya viwango vyao na baada ya muda mfupi wakapoteza zote. Kuna watu wameshawahi kushinda bahati nasibu na kupata fedha nyingi na watu wakaamini kuwa wameshashinda maisha, lakini baada ya muda mfupi fedha zote zikaisha na wakarudia maisha yao ya kawaida.

Ndugu uwezo wako haujaishia hapo, unayapata matokeo hayo kwa sababu ya viwango ulivyojiwekea. Huwezi ukaenda mbali ya hapo mpaka utakapoiruhusu akili yako kuamini viwango vya juu zaidi. Ni sawa na mbuzi aliyefungwa kamba kwa ajili ya  malisho, hawezi kwenda kula mbali zaidi ya urefu wa kamba yake. Ili aweze kwenda mbali zaidi, inabidi aongezewe urefu wa kamba yake au afunguliwe na kuachiwa huru.


Kupandisha viwango ni kukubali kuishi maisha ya aina nyingine. Haya ni maisha ambayo hayafanani na maisha ambayo umezoea kuishi na kupata matokeo ulidumu kwa muda mrefu. Kupandisha viwango ni hatua za kutumia uwezo wako kwa kufanya vitu vigeni au vilevile kwa viwango vya juu zaidi. Zifuatazo ni hatua za kuchukua ili kuweza kupandisha viwango vya mafanikio yako:

Amini kuwa unaweza kupata matokeo zaidi ya hayo.


 Mwimbaji na mwanamitindo Mrilyn Munroe alisema ‘’The sky is not the limit. But your mind’’ akimaanisha kuwa anga haliwezi kuwa kikwazo bali akili yako. Kama bado upo hai hakuna kikwazo chochote kinachoweza kukuzuia kupata kile unachotaka. Ukiwa ardhini na ukainua macho yako juu utaona kama kuna mwisho unauona, lakini kumbe unaweza ukatoka kwenye sayari ya dunia na kwenda masi. Hivyo hakuna kinachoweza kukuzuia kwenda na kufanya chochote kipindi cha uhai wako. Angalia ulipo sasa na ona kuwa kuna nafasi ya kwenda juu zaidi kwa sababu uwezo huo upo ndani yako, ni jukumu lako tu kuuamsha.


Weka viwango vya juu zaidi.

Bado una uwezo ndani yako ambao bado hujautumia. Unaweza kuutumia uwezo huo kufanya mambo makubwa zaidi ya yale uliyokwisha kuyapata. Mwandishi Napoleon Hill aliandika kuwa “Whatever Your Mind Can Conceive and Believe, It Can Achieve.”  Akimaanisha kuwa chochote ambacho akili yako inakiridhia kitafikiiwa. Akili ni  yako, na kazi ambayo itapanga itafanikiwa kwa sababu tayari uwezo huo upo ndani yake.  Usiogope kuweka viwango vikubwa, uwezo wa kuvifikia viwango hivyo upo, wewe iruhusu akili yako iamini.

Weka mikakati ya ya kufikia viwango hivyo.


Viwango ulivyoweka ni malengo ambayo yanahitaji mikakati ili kuyafikia. Kwa sababu viwango vya sasa ni vikubwa kuliko ulivyozoea, unahitaji kuweka nguvu zaidi na kufanya tofauti na mazoea. Vile ulivyozoea kufanya ndiyo kumekufikisha hapo ulipo, ili uweze kupata matokeo ya utofauti huna budi kufanya tofauti na mazoea. Ndiyo maana mwanasayansi nguli Albert Einstein anasema “Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results.” Akimaanisha kuwa wazimu ni kufanya jambo kitu hicho hicho kila wakati na ukitarjia kupata matokeo tofauti. Hii ni kauli ambayo inakukumbusha kuwa itakulazimu kubadilika ili uweze kupata matokeo baaday kuweka viwango vya juu.

 Mbinu na nguvu zaidi zitkazohitajika kwa ajili ya kupata matokeo ya viwango vya juu zaitaamusha uwezo wako ndani. Hivyo usihofu utatimizaje malengo makubwa uliyojiwekea. Vipaji vyenye uhusiano na uwezo wako vitaanza kutumika vyema kwa kuw ana viwango vikubwa. Utahitaji maarifa zaidi ili kuweza kutimiza viwnago vikubwa ulivyojiwekea. Pata muda wa kusoma zaidi kuhusu yale unayotarajia kuyafanya pia hudhuria semina na kujifunza zaidi. Kila unachojifunza hakikisha unakiweka kwenye matendo hapo ndipo itakuwa rahisi kukabiliana na changamoto utakazokutana nazo.

Ndugu, una nafasi ya kupandisha viwango katika eneo lolote la maisha yako; uchumi, afya, mahusiano, kazi nk. Weka malengo yako leo ya kupandisha viwango vya maisha yako. Kadri unavyopandisha viwango hivyo kila siku ndivyo unavyozidi kuboresha maisha yako. Kila utakapokuwa unapanda ngazi ndivyo utakavyokuwa unaelekea na kukaribia kilele cha mafanikio ya maisha yako.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *