Hii Ni Akili Ya Simba Unayoweza Kuitumia Kuanzisha Na Kukuza Biashara.


Categories :




Hii ni taarifa iliyonisikitisha baada ya kuisikia! Asilimia 96 ya biashara mpya zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya miaka 10. Asilimia 80 ya biashara mpya zinazoanzishwa hufa ndani ya miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Na hata ile asilimia 4 ya biashara zinazovuka miaka kumi, siyo zote zinakuwa zinajiendesha kwa faida, imetokea tu zimeepuka kifo. Hii naamini inakusikitisha na wewe.

Inawezekana kwenye orodha ya biashara hizo zilizokufa na ya kwako imo! Kwenye miaka mitano umeanzisha na kufunga biashara ngapi? Kuna watu kila mwaka wanaanzisha biashara mpya, je na wewe ni miongoni mwao?

Kuna kitu kilichokosekana kwa waanzisha biashara hizo zinazokufa ambacho kipo ndani ya simba. Ni kitu gani hicho kipo ndani ya simba ambacho waanzisha biashara wanakikosa? Kitu hicho ni SHAUKU.

Ukimuangalia simba siuo mrefu kama twiga, wala siyo mkubwa kama alivyo tembo, wala hana rangi nzuri kama pundamilia lakini licha ya kukosa vitu vyote hivyo, simba ndiye mfalme wa mwituni. Huyo ndiye mnyama anayewatawala wanyama wengine wote. Licha ya udogo wake, lakini anaweza kumla tembo aliye mkubwa. Nini kinachomfanya aweze kutawala wanyama wengine wote? Nini kinamfanya amle tembo? Ni shauku anayokuwa nayo akitaka kuwapata.

Simba anapomuona tembo haoni utisho wa ukubwa wa tembo, bali huona kitoweo kikubwa kilichopo mbele yake. Kitu pekee atakachopenda akipate na atahakikisha anakipata ni kitoweo hicho. Ni shauku hii ndiyo inayomfanya aamushe uwezo wake ndani yake kupambana na tembo mpaka amuue na kufanya kitoweo.



Hii ni shauku ambayo mfanyabiashara yoyote inabidi awe nayo anapoianzisha, kuikuza na kuilinda biashara yake. Kitu gani kinachokusukuma kuanzisha yako? Je ni kwa kiasi gani unaipenda biashara yako?

Ndugu safari ya kujenga biashara ya mafanikio ni ndefu na ngumu, na hii ndiyo sababu mojawapo ambayo inawafanya watu wengi kuishia njiani. Wanaofanikiwa kujenga biashara zenye mafanikio ni wale tu waliojenga shauku kubwa ndani yao za kuhakikisha wanakuwa na biashara zenye mafanikio.

Kitu kimojawapo kinachokufanya uwe na shauku kubwa ya kuijenga biashara yenye mafanikio licha ya changamoto zitakazojitokeza ni kuanzisha biashara kutoka kwenye kile unachokipenda. Mtandao wa AmshUwezo umekuandalia semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kiundani namna ya kujenga shauku kubwa kwenye biashara unayoifanya ili uweze kujenga biashara yenye mafanikio licha ya changamoto zilizopo. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.

Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7

Wakati wa kufaidi utele wa dunia umefika. Usipange kukosa fursa hii.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *