Hii Ndiyo Biashara Yako Inayolipa!
Nataka kufanya biashara, ni biashara gani inalipa kwa sasa? Ni biashara gani inakutoa haraka? Ni biashara gani haina heka heka? Baishara gani inayowatoa watu wengi? Nina mtaji, nifanye biashara gani? Haya yamekuwa miongoni mwa maswali ambayo watu wengi wanajiuliza pale wanapotaka kuanzisha biashara biashara.
Mara nyingi maswali haya yamekosa majibu sahihi. Licha ya kujiuliza maswali haya muhimu lakini mwisho wa siku wameaanzisha biashara ambazo zimekufa baada ya muda mfupi tu. Wengine baada ya kukosa majibu sahihi wameishia kuiga biashara zinazofanywa na watu wengine.
Imekuwa ni kawaida mtu kuangalia biashara gani inayoonekana kulipa kwa jirani na yeye kuanzisha hiyohiyo akiwa na uhakika kuwa na yeye itamlipa. Lakini wengi wamepata matokeo tofauti na matarajio na mara nyingine wamefikiria wale waliotangulia kuanzisha biashara hizo wanawaroga.
Ndugu yangu, hakuna biashara moja inayomfaa kila mmoja. Biashara inayofanya vizuri kwa mfanyabiashara A inaweza isifanye vizuri kwa mtu B. Unapoamua kuiga biashara anayoifanya mtu fulani tambua kuna uwezekano mkubwa wa biashara hiyo kuwa ngumu kwako.
Kumbe biashara inayokulipa wewe iko wapi? Biashara inayokulipa wewe ipo ndani yako, ndiyo ndani yako. Kumbuka biashara ambayo unaweza kuianzisha, kuikuza na kuilinda mpaka ikufikishe kwenye mafanikio makubwa inatokana na msukumo mkubwa kutoka ndani yako. Hii ni biashara ambayo utakuwa tayari kustahimili changamoto zote zitakazosimama.
Hivyo biashara yako inayolipa inatokana na vitu vile unavyovipenda kuvifanya. Vitu gani unapenda kuvisikia au kuviona mara kwa mara na akili ya yako inalipuka kwa tamaa? Je ni fasheni za mavazi? Je ni michezo? Hivi ni vitu vinavyotoka ndani mwako. Lakini pia kuna vitu ambavyo upo tayari kuvifanya hata kama hulipwi! Huko ndiko wazo bora la biashara bora kwako ndiko linakotokea.
Biashara inayokulipa inaanza na wazo bora la biashara. Wazo bora la biashara yako linatoka ndani mwako na sio kwa kuiga kutoka kwa mtu mwingine.
Kujua vitu unavyovipenda kuona au kusikia au kuvifanya hata bila malipo, ni hatua ya kwanza kabisa kwenye kupata biashara inayomfaa. Kuna hatua nyingine tatu ili kukamilisha hatua hizo na mwisho kupata wazo bora kabisa la biashara ambayo itakupa mafanikio makubwa.
Ndugu! Mtandao wa AmshUwezo unakujali sana na unatamani upate wazo la kuanzisha biashara bora itakayokupa mafanikio makubwa. Hivyo imeandaa semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kiundani hatua nne muhimu za kupata wazo bora la biashara kisha kuianzisha na kukikuza na kupata mafanikio ya ndoto yako. Pia itakuwa fursa kwa wewe ambaye tayari una biashara kuboresha biashara yako kwa kupitia hatua hizo nne ili kuwa na mtazamo bora zaidi wa biashara yako. Hii itakuwa chachu ya kukuza biashara yako.
Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.
Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.
https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7
Wakati wa kufaidi utele wa dunia umefika. Usipange kukosa fursa hii.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz