Hivi Ndivyo Unavyoweza Kufanikiwa Kwa kufanya Vyote Pamoja.


Categories :

Ajira kwa sasa imekuwa sio njia ya uhakika kwa sasa ya kufikia utajiri. Ule ushauri wa kuwa nenda shule, kasome kwa bidii, faulu vizuri, ajiriwa na kupata kazi nzuri na kisha utapata fedha na kuwa na maisha mazuri umepitwa na wakati. Huu ulikuwa ni ushauri uliokuwa unalipa zamani  kwenye zama za viwanda ambapo watu waliokuwa wamesoma na kuwa na ujuzi walikuwa wachache na hivyo kuwa na thamani kwenye ajira.

Lakini ushauri huu unaonekana kupitwa na wakati kwa sasa ambapo idadi ya watu waliosoma na kuwa na ujuzi ni wengi. Pia maendeleo ya sayansi na teknolojia yamepunguza sana uhitaji wa wafanyakazi. Sababu hizi zimefanya watu wengi wenye sifa za kuajiriwa kutokuwa na nafasi kuajiriwa. Ndiyo maana sio ajabu sasa kuona kuna watu wengi ambao hawana ajira licha ya kusoma na pia uhakika wa kubaki kwenye ajira umekuwa ni mdogo sana.

Kwa sababu hiyo kuwa kwenye ajira huku ukitegemea kipato cha ajira hiyo pekee ni kujiweka kwenye mazingira hatari sana kiuchumi. Kutegemea chanzo kimoja cha kipato ni kuwa mtumwa, kwani itakuhitaji kwa namna yoyote uibembeleze ajira yako ili uendelee kubaki.  Njia pekee ya kuondoa utegemezi huu wa ajira na kuwa huru ni kuwa na chanzo kingine cha kipato. Njia moja yenye uhakika ni kuwa na biashara yenye mafanikio.

Swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wakati gani waanzisha biashara wakiwa kwenye ajira? Je waache ajira na kuanzisha biashara? Je wasubiri mpaka wastaafu kisha waanzishe ajira?  Au wafanye vyote? Njia sahihi ya kupata uhuru wa kifedha ukiwa kwenye ajira ni kuamua kuanza kufanya vyote; yaani ajira na biashara.

Baadhi ya faida za kufanya vyote ni kuepuka utumwa wa kipato kimoja, kuweza kuilea biashara vizuri hasa inapokuwa changa, kuweza kutengeneza mtandao wa biashara na wafanyakazi wenzako, kuwa na uwezo wa kujaribu biashara mbalimbali nk. Biashara yenye mafanikio haikui kama uyoga au mchicha, inahitaji muda kuianzisha kuikuza na kuvuka changamoto nyingi mpaka kufikia mafanikio makubwa. Hivyo kuilea na kuifikisha kwenye mafanikio makubwa inaweza kuwa rahisi kama utakuwa bado upo kwenye ajira na unaendelea kupata kipato kingine.

Hofu ya kushindwa kufanya vyote yaani ajira na biashara imekuwa sababu mojawapo ya watu wengi kutothubutu kuanzisha biashara wakiwa kwenye ajira. Pia wapo walianzisha biashara kadhaa lakini wakaishi njiani. Ufanye nini ili uweze kufanikisha hili? Mtandao wa AmshaUwezo umekuandalia  semina ya siku kumi kuanzia Tar 11 – 20 Julai 2022 yenye maada ya semina hii ni UWEZO WA KUAZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Kupitia semina hiyo utapata nafasi ya kujifunza kiundani namna ya namna ya kupata wazo na kuweza kuanzisha biashara yenye mafanikio ukiwa bado upo kwenye ajira. Kila siku asubuhi litawekwa somo la siku kwenye kundi maalumu la wasap, utalisoma na kuchukua hatua kisha jioni kutakuwa na nafasi ya majadiliano ya mwalimu na washiriki wote ili kulielewa somo hilo vizuri na kulitumia.

Gharama za kushirikia somo hili ni shilingi elfu kumi (sh 10,000/) tu ambayo unalipia kupitia namba 0752206899/0714301952(Alfred Mwanyika). Ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina hii jiunge leo kwa kubonyeza kiunganishi hapo chini.

https://chat.whatsapp.com/CaoS3cbLqasJWIbPzcoyi7

Hii ni fursa ya kuepuka utumwa wa kipato kimoja.  Usipange kukosa nafsi hii.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,

Kocha na Mwalimu wa uwezo wako halisi,

Mawasiliano;

Simu; 0752206899/0714301952

Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz

Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *