Category: HAMASA

Hii Ndiyo Biashara Yako Inayolipa!Hii Ndiyo Biashara Yako Inayolipa!

Nataka kufanya biashara, ni biashara gani inalipa kwa sasa? Ni biashara gani inakutoa haraka? Ni biashara gani haina heka heka? Baishara gani inayowatoa watu wengi? Nina mtaji, nifanye biashara gani? Haya yamekuwa miongoni mwa maswali ambayo watu wengi wanajiuliza pale wanapotaka kuanzisha biashara biashara. Mara nyingi maswali haya yamekosa majibu [...]

Hii Ni Akili Ya Simba Unayoweza Kuitumia Kuanzisha Na Kukuza Biashara.Hii Ni Akili Ya Simba Unayoweza Kuitumia Kuanzisha Na Kukuza Biashara.

Hii ni taarifa iliyonisikitisha baada ya kuisikia! Asilimia 96 ya biashara mpya zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya miaka 10. Asilimia 80 ya biashara mpya zinazoanzishwa hufa ndani ya miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Na hata ile asilimia 4 ya biashara zinazovuka miaka kumi, siyo zote zinakuwa zinajiendesha kwa faida, imetokea [...]

Hata Wewe Una Uwezo Huo.Hata Wewe Una Uwezo Huo.

Mimi sio mtu wa kufanya biashara! Biashara zina wenyewe bwana. Biashara za kabila fulani, biashara za uko fulani. Biashara zina wenyewe bwana. Haya ni maneno ambayo huwa yanasikiwa yakisemwa na watu. Watu hawa wanaamini kuwa kuna watu fulani ambao ndiyo wanaostahili kufanya biashara. Yaani hata kama kuna watu wengine tofauti [...]

Wewe Pia Una Sehemu Katika Utele Huu.Wewe Pia Una Sehemu Katika Utele Huu.

Licha ya simba kuendelea kuwawinda na kuwala swala kila siku swala hao hawajawahi kuisha. Licha ya watu kuvua na kula samaki kila siku lakini bahari haijawahi kuishiwa samaki. Licha ya wanyama kuendelea kuvuta hewa ya oksjeni kila siku lakini hewa hiyo haijawahi kuisha. Hivi ni baadhi ya viashiria vya kuwa [...]

Unaweza Kukipata Hiki Ulichokitamani Kwa Siku Nyingi.Unaweza Kukipata Hiki Ulichokitamani Kwa Siku Nyingi.

Kuna kitu ambacho ni tamanio la karibu kila mtu hapa duniani. Kitu hicho kimekuwa kikichukua muda mwingi wa maisha ya mtu kutafutwa. Na mambo mengi ya mtu huyo hukaa vizuri akishakipata kitu hicho. Akishakipata na yeye huona wa thamani hapa duniani. Naamini unatamani ujue kitu hicho, nami nakuambia kuwa kitu [...]

SEMINA! SEMINA!   UNAWEZA KUTENGENEZA UTAJIRI WAKO SASA.SEMINA! SEMINA!   UNAWEZA KUTENGENEZA UTAJIRI WAKO SASA.

MADA:   UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA YENYE MAFANIKIO. Je yamekuwa ni matamanio yako ya siku nyingi kuwa na biashara yenye mafanikio makubwa lakini kila ukifikiria biashara gani uifanye lakini hupati wazo? Je umeanzisha biashara nyingi lakini hakuna iliyokua na kukupa mafanikio lakini zimeishia kufa? Je una biashara ambayo inapumulia [...]

Huu Ndiyo Ufunguo Wa Kupata Matokeo Ya Tofauti.Huu Ndiyo Ufunguo Wa Kupata Matokeo Ya Tofauti.

Kuna matokeo unayoyapata ambayo yanakuudhi? Kuna matokeo ambayo umeyatamani siku nyingi lakini huyapati? Utaanzia wapi? Kuna sehemu moja ambayo inabidi uianzie ili uweze kupata matokeo yoyote yale. Kupata matokeo ambayo huyapati sasa, ni lazima ufanye mabadiliko, yaani ufanye kitu tofauti na kile ulichozoea. Kwa kufanya kwa utofauti kunaweza kuwa kufanya [...]

Pandisha Ngazi Kupanda Kileleni.Pandisha Ngazi Kupanda Kileleni.

Hatua ya mafanikio ya maisha uliyofikia ni kwa sababu ya viwango ulivyojiwekea maishani mwako. Viwango hivyo ndiyo ndivyo vinavyoamua ufanikiwe kiasi gani kwenye kila nyanja ya maisha yako.  Viwango hivyo ndivyo vinavyoweka ukomo kwenye  mafanikio unayoyapata, hii ndiyo sababu ya kwa nini muda umezidi kwenda lakini bado upo pale pale. [...]

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Kesho Yako Leo.Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Kesho Yako Leo.

“Msitu wa miti unaouona leo ni matokeo ya miche iliyopandwa na kulindwa kwa miaka mingi hapo nyuma” Maisha yako ya leo sio ya leo bali ya miaka mingi ya nyuma. Kile ulichokuwa unakifanya miaka kadhaa iliyopita ndicho kilichokupa maisha yako ya leo. Kama unafurahia maisha yako leo ujue kwa asilimia [...]

Kwa Nini Unajifungia Mwenyewe?Kwa Nini Unajifungia Mwenyewe?

Binadamu ameshindwa kutumia hazina kubwa ya uwezo ndani yake kwa sababu ya ukomo anaojiwekea. Wapo watu wanaoendelea kuendesha magari ambayo wao wanatafsiri ni ya kawaida huku wakiishia kutamani magari mazuri. Ukimwuliza kwa nini hamiliki gari hilo anasema yeye hufanana na gari hilo. Gari hilo zuri ni watu wa daraja fulani [...]