Category: HAMASA

Umeshindwa Si Kwa Sababu Ya Kutokufahamu, Ila Kwa Sababu Hii…Umeshindwa Si Kwa Sababu Ya Kutokufahamu, Ila Kwa Sababu Hii…

Ni muda mrefu sasa tangu umekuwa na matamanio ya kupata mafanikio fulani katika maisha yako. Ni muda sasa tangu ulipohamasika kuchukua hatua fulani lakini baada ya hapo shauku hiyo imekuwa ikishuka kila siku, na mpaka sasa hakuna ulichokifanya. Ni muda mrefu umepita tangu umekuwa na wazo la kuanzisha au kukuza [...]

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutambua Uwezo Wako Ulionao na Kupata Utajiri.Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutambua Uwezo Wako Ulionao na Kupata Utajiri.

“Ni mpaka nazi ivunjwe ndipo uone kitu chenye thamani ndani yake. Kadhalika ni mpaka yai lipasuliwe ndipo unaweza kupata kimiminika chenye thamani ndani yake”Thamani ya vitu ipo ndani, mara nyingine ni vigumu kuiona thamani hiyo mpaka upate nafasi ya kuchungulia ndani. Kama huifahamu nazi, huwezi ukaijua kwa haraka haraka kama [...]

Utapata Unachokitaka Kuanzia Sasa.Utapata Unachokitaka Kuanzia Sasa.

Ni muda umepita tangu umezaliwa, ni muda mrefu tangu umehitimu masomo yako, ni muda mrefu tangu umeondokewa na wategemezi wako, ni muda mrefu umepita tangu umeanzisha biashara lakini hujaanza kupata faida; hali hizi zimekufanya ujisikie kama umefika mwisho kwani huoni nini ufanye ili usonge mbele. Sasa nifanye nini? Ninaanzia wapi? [...]

Furaha Yako Ya Kweli Hailetwi Na Ndege.Furaha Yako Ya Kweli Hailetwi Na Ndege.

“Rangi ya nje ya chupa ya maji haiwezi kubadili rangi ya maji ndani yake” Kwa kawaida maji masafi hayana rangi. Hivyo mwonekano wa maji yakiwekwa kwenye chupa hutegemea rangi ya chupa hiyo. Yakiwekwa kwenye chupa nyekundu, nayo yataonekana mekundu, yakiwekwa kwenye chupa ya bluu, kadhalika nayo yataonekana ya bluu. Licha [...]

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukimbia Hata Kama Huioni Miguu Yako.Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukimbia Hata Kama Huioni Miguu Yako.

“Licha ya jongoo kuwa na miguu mingi lakini hushindwa kasi na nyoka ambaye hana hata mguu mmoja”Kama uwingi wa miguu ungekuwa ndiyo kigezo pekee cha kasi ya kutembea, basi jongoo angekuwa na kasi hata ya kuzidi kasi ile ya farasi. Lakini licha ya jongoo kuwa na miguu mingi bado ana [...]

Hivi Ndivyo Umekuwa Ukizima Moto Kwa Petroli.Hivi Ndivyo Umekuwa Ukizima Moto Kwa Petroli.

Petroli si inawaka! Itatumikaje tena kuzima moto? Inawezekana huu ni mshangao na swali ulilojiuliza baada tu ya kusoma kichwa cha makala hii. Lakini inawezekana wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakifanya hivyo. Endelea kusoma ujue ni kwa namna gani umekuwa ukizima moto kwa petroli. Petroli ni miongoni mwa mafuta [...]

Mtoto Anayelia Sana Ndiye Anayenyonyeshwa.Mtoto Anayelia Sana Ndiye Anayenyonyeshwa.

Mbinu kuu anayotumia mtoto kueleza nini anachojisikia au anachokitaka ni kulia. Hata wakati wa kuzaliwa, ili aonekane amezaliwa kawaida inampasa alie, na asipo lia kwa hiari hulazimishwa kulia. Mtoto anapolia mama au mlezi hujua mtoto ana jambo ambalo linamsibu na hana budi kumchunguza au kujua ni nini anakitaka ile apewe. [...]

Kama Bado Upo Hai, Bado Hujachelewa.Kama Bado Upo Hai, Bado Hujachelewa.

Katika maisha yako kuna mtu wa aina fulani ulitamani uwe lakini mpaka sasa hujawa mtu huyo. Katika maisha yako kuna hali fulani ya kifedha ulitamani uifikie ili uwe huru, lakini hujaifikia licha jitihada unazoweka. Katika maisha yako kua maeneo fulani ya dunia ulitamani uyafikie kabla hujaiaga dunia, lakini mpaka sasa [...]

Huu Ndiyo Msingi Imara Wa Nyumba Ya Utajiri Wako.Huu Ndiyo Msingi Imara Wa Nyumba Ya Utajiri Wako.

Nyumba imara hujengwa juu ya msingi imara. Wengi hupendezwa na rangi za kuta za nyumba zinazoonekana baadaye, lakini uimara wa hizo kuta zitategemea ni kwa uimara gani msingi huo ulijengwa. Hivyo uimara au ubovu wa nyumba hutegemea msingi wa nyumba hiyo. Mara nyingi msingi wa nyumba huwa hauonekani na hivyo [...]

Unaweza Kushinda Mashindano Hata Kwa Kutanguliza Pua Tu!Unaweza Kushinda Mashindano Hata Kwa Kutanguliza Pua Tu!

Farasi wengi wanapokuwa kwenye mashindano, mshindi hupatikana kwa kuangalia nani anayezidi wenzake baada ya umbali  wa kukimbia mashindano kukamilika. Mara nyingine hutokea mmoja kuwazidi wenzake kwa pua yake kutangulia kuliko wenzake na hivyo yeye kutunikiwa ushindi. Hili ni funzo kubwa sana katika maisha yetu ya ushindi, huwa tunafikiria kuwa ili [...]