Category: USTAHIMILIVU

Usikatishe Safari Kwa Sababu Umepitwa….Usikatishe Safari Kwa Sababu Umepitwa….

Kama utakuwa kwenye gari la abiria halafu ghafla dreva akasimama na kusema tunaahirisha safari kwa sababu kuna gari linelipita(overtake) gari lake na yeye hapendi hilo, ungemshangaa sana. Kama ungemuona mwanariadha ameacha mashindano kwa sababu tu kuna mtu amempita na yeye hakupenda hilo, ungemshangaa sana. Inawezekana ungemuuliza kama kweli alidhamiria mashindano [...]

0 Comment| 7:53 pm

Pale mtu anapolia machozi ni rahisi sana mtu mwingine kuyaona machozi hayo yakitiririka kutoka machoni kwenda mashavuni hata mpaka kwenye kidevu. Kama kuna mtu amekuwa akikusubiri upate shida afurahi ni rahisi sana kutambua kuwa muda wake umefika wa yeye kufurahi. Kadhalika kama kuna mtu alikuwa anakutegemea wewe kama shujaa wake, [...]

Je Ungependa Kupata Matokeo Yenye Kishindo? Basi Muulize Tembo Huyu…..Je Ungependa Kupata Matokeo Yenye Kishindo? Basi Muulize Tembo Huyu…..

Mbwa na na tembo walikubaliana wabebe mimba kwa wakati mmoja ili waweze kuendeleza vizazi vyao. Baada ya miezi mitatu tu mbwa alizaa watoto 6. Alikaa miezi mitatu akashika mimba tena na kuzaa watoto wengine 12 baada ya miezi 9 akazaa watoto wengine 12 baada ya miezi 12 akawa na mimba [...]

Kwani Wewe Umejaribu Mara Ngapi?Kwani Wewe Umejaribu Mara Ngapi?

Kila kitu ninachokifanya hakitiki! Kwani umejaribu mara ngapi? Mimi nyota yangu imefifia inabidi niende kwa mtaalamu aisafishe, mambo yangu hayaendi! Kwa umejaribu mara ngapi? Nilitaka kuwa mbobezi kwenye eneo hili lakini naona kama nipo palepale. Kwa wewe umefanya kwa muda gani? Nimefanya muda mrefu sana lakini sipati majibu, sasa naacha. [...]

Huu Ndiyo Wakati Wa Kuonyesha Imani Yako!Huu Ndiyo Wakati Wa Kuonyesha Imani Yako!

Mambo mengi kama siyo yote ya msingi utakayokuwa unafanya maishani mwako hayatakuwa na majibu ya papo kwa papo. Hivyo unanitaji kusubiri ndipo uone matokeo. Kuna matokeo yatachukua muda mfupi kutokea, wakati mengine yakichukua muda mrefu. Kwa sababu ya matokeo kuchelewa, kuna watu wamekosa uvumilivu kisha kukata tamaa. Lakini kwa sababu [...]

Una Machaguo Mawili, Fanya Uchaguzi Bora!Una Machaguo Mawili, Fanya Uchaguzi Bora!

Katika kuisi maisha yako una machaguo mawili, huna budi uchague moja. Uchaguzi wako leo ndiyo huamua nini ukipate kesho. Chaguo la kwanza ni kuchukua hatua sahihi zenye maumivu kisha upate unachokitaka na kustahili. Chaguo la pili ni kuyakwepa maumivu ya kufanya kitu sahihi sasa, lakini kuja kukutana na maumivu ya [...]

Dhoruba Inakuja, Simama Hapa Usianguke!Dhoruba Inakuja, Simama Hapa Usianguke!

Uimara wa nyumba hupimwa wakati wa dhoruba. Sifia nyumba yako kwa uzuri na uimara wake, lakini sifa hizo zitathibitika pale mafuriko na pepo kali vitakapokuja. Uimara wa nyumba huanzia kwenye msingi wake. Nyumba iliyojengwa kwenye msingi imara, hustahimili mafuriko na pepo kali. Licha ya mafuriko na pepo kali kuifikia nyumba, [...]

Hii Ni Tabia Inayozidi Hata Kipaji.Hii Ni Tabia Inayozidi Hata Kipaji.

Ukimuona mtu anayeanza kuponda jiwe kwa nyundo, unaweza kumuonea huruma au kumkatia tamaa. Kwani wataki atakapokuwa anashusha nyundo zile za kwanza, jiwe litaendelea kumwangalia tu bila y ahata kuonyesha dalili kuwa litapasuka. Lakini kuna kitu cha ajabu sana hutokea pale ambapo mpondaji anapokuwa mvumilivu na mstahimilivu akiendelea kushuka nyundo juu [...]

Njia imefungwa. Pita huku!Njia imefungwa. Pita huku!

Njia imefungwa! Pita kulia! Pita kushoto! Haya ni maandishi unayoweza kukutana nayo kwenye barabara ambayo umezoea kuipita. Kukiwa na matengenezo kwenye barabara uliyozoea kupita, barabara hiyo hufungwa ili kupisha ukarabati huo. Lakini mamalaka huwa haziachi watumiaji wateseke, badala yake hutafuta namna ya kuwawezesha kuendelea na safari. Huandaa njia nyingine na [...]

Kama Unataka Kufanikiwa, Usiige Alichokifanya Huyu Bwana Misosi.Kama Unataka Kufanikiwa, Usiige Alichokifanya Huyu Bwana Misosi.

Leo kuna harusi tatu! Watanikoma! Haya ni maneno ambayo jamaa mmoja maarufu kijijini alijisemea moyoni baada ya kuambiwa kuna harusi tatu kijijini hapo. Umaarufu wa huyu jamaa ulikuwa ni kwenye kupenda kula sana. Alipenda kula kuliko kitu kingine chochote. Wanakijiji walioamua kumbatiza jina jamaa huyo na kumuita bwana misosi. Ilikuwa [...]