Utafanikiwa Kumla Ng’ombe Mzima Kama Utamkata VipandeUtafanikiwa Kumla Ng’ombe Mzima Kama Utamkata Vipande
Kila mtu aliyepo hapa duniani ana uwezo wa kipekee wa kufanya mambo makubwa ambayo huachwa kama alama ya yeye kuwepo hapa duniani. Anayefanikiwa kufikia mafanikio makubwa ni yule anayetengeneza ndoto kubwa na kufanikiwa kuiishi kikamilifu. Ndoto kubwa hutimia kwa kuiwekea malengo. Kadri unavyokuwa na ndoto kubwa ndivyo inavyohitaji kuwa na [...]
Sifa Tano(5) Za Malengo Bora Yatakayokufikisha Kwenye Mafanikio MakubwaSifa Tano(5) Za Malengo Bora Yatakayokufikisha Kwenye Mafanikio Makubwa
Licha ya ndege kuwa angani kwa kimo kirefu kutoka ardhini lakini rubani wake hufanikiwa kusafiri maili nyingi na kuifikisha ndege hiyo bila ya kupotea. Hii ni kwa sababu hutumia dira iliyopo kwenye chombo hicho kukiongoza kwa usahihi. Kadhalika treni huhitaji reli ambayo itaiongoza kwa kupita juu yake na kufika inakotarajiwa [...]
Mambo Matano(5) Ya Kufanya Baada Ya Kuchelewa Kuanza KuishiMambo Matano(5) Ya Kufanya Baada Ya Kuchelewa Kuanza Kuishi
Maisha ya mwanadamu yapo kwenye muda tangu kuzaliwa kwake mpaka anapokufa. Katika kipindi hicho ndipo anapotarajiwa kuishi maisha yake. Historia anayoiacha duniani baada ya kufa hutegemea kile alichokifanya kipindi cha uhai wake. Bahati mbaya baada ya kufa hawezi kuibadili historia yake. Binadamu huwa na mipango mingi sana wakati anaendelea kuishi [...]
Ikimbize Siku, Usiiache IkukimbizeIkimbize Siku, Usiiache Ikukimbize
Moja ya vitu vinavyolalamikiwa na watu wengi ni ufinyu wa muda. Limekuwa lalamiko la watu kuwa muda hautoshi. Kila unayemuuliza kwa nini hafanyi kitu fulani, atakwambia hana muda. Kwa mfano kwa nini watu wengi hawasomi vitabu vya kuongeza maarifa ya maisha yao binafsi au kuhusu kazi zao, watakuambia hawana muda. [...]
Tengeneza Mtazamo Kisha Weka ViwangoTengeneza Mtazamo Kisha Weka Viwango
Kuna chujio lipo katikati ya vitu halisi na macho ya binadamu. Chujio hilo ni mtazamo. Vitu vingi unavyoviona si katika uhalisia wake bali kulingana na chujio hilo. Kumbe watu wawili wanaweza wakakutana na jambo moja lakini wakawa wanaona tofauti. Hii ni sababu mojawapo ya watu kutofautiana viwango vya mafanikio hata [...]